Jifunze mbinu za kufanikiwa kimasomo

Jifunze mbinu za kufanikiwa kimasomo

JIFUNZE MBINU ZA KUFANIKIWA KIMASOMO

Mambo vipi mwanafunzi, natumaini u mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kawaida ya hapa na pale.

Basi leo katika karia tumekusogezea mbinu tano ambazo wewe mwanafunzi wa chuo kama ukizitumia utaweza kupata mafanikio katika masomo yako.

Natambua kuwa hakuna hata mwanafunzi mmoja anayependa siku ya mwisho apate matokeo mabaya hata kwa wale wasiosoma pia huwa wanapenda kupata matokeo mazuri.

Wanafunzi wengi kwa namna moja ama nyingine huwa wanakuwa wanakipindi kigumu wanasoma kwa bidii lakini mwisho wa siku wanapata ambacho hawajatarajia, wengine wamekuwa wanashindwa kuelewa mbinu gani watumie ili waweze kupata mafanikio katika masomo yao.

Mambo ya msing ya kufuatilia ili kupata mafanikio katika masomo yako kwanza;

MTANGULIZE MUNGU MBELE

Ndio unapaswa kumtanguliza Mungu katika masomo yako ili uweze kufanikiwa kielimu. Mungu ndio kila kitu hivyo hakikisha unajenga tabia ya kuombea masomo yako kila siku na kila mara.

Kila siku unapoamka asubuhi kabla ya kwenda chuo piga goti na kuomba, mwombe Mungu akutangule katika kila kitu kwenye maSomo yako, mwombe akupe wepesi wa uelewa, akupe umakini na akuepushe na maroho yote machafu yatakayokutoa katika hali ya utulivu na kushindwa kuwa katika mood nzuri.

Watu wengi tunashindwa kuelewa kuwa zipo roho chafu zinazotuzuia katika malengo tunayojiwekea katika masomo yetu, wapo wengi wamekuwa wanasumbuliwa na magonjwa yasiyofahamika haswa wakati wa masomo, kukosa hamu ya kusoma, kichwa kuwa kizito kuelewa.

Suluhisho ni kuhakikisha unasimama katika maombi ili Mungu aweze kusimamia masomo yako, Kumbuka Mungu anatuambia tukamate sana elimu tusimwache aende zake, kwa wale wa wakristo soma biblia methali 4:13.

Tambua mpango wa Mungu sio kufeli ndio maana mungu yeye mwenyewe anataka tusome kwa bidi.

HAKIKISHA UNAENDA NA MUDA

Muda ni tatizo kubwa kwa wanafunzi, wengi hawajui kuendana na muda matokeo yake muda umekuwa ukiwatupa mkono.

Jambo la kwanza la msingi mwanafunzi siku ya kwanza unafungua chuo jua masomo ndio yameanza hivyo, anza kuweka malengo mwanzoni kabisa usisubiri siku ziende mambo yatakuwa mengi  utaanza kusoma kwa presha.

Wanafunzi wengi wamekuwa wakizembea mwanzoni ,mwishoni wanakujakushtuka mtihani imekaribia,wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kusoma kwa presha na kukuta wanapata matokeo ambayo hawataki kuyapata.

Hakikisha unakuwa na timetable ya masomo mwanzoni kabisa chuo kinapofunguliwa ili uweze kuendana na muda,jua kabisa muda unaouchezea mwanzoni utakugharimu siku za mwishoni.

Epuka kusoma kwa presha hakikisha unakuwa na maandalizi ya kutosha toka mwanzoni.

JIAMINI UNA UWEZO WA KUTOSHA

Wanafunzi wengi wamekuwa hawajiamini na uwezo wao Mungu aliowajalia, baadhi yao wanaamini uwezo wao mdogo ndio maana wanashindwa kufanya vizuri katika masomo yao. 

Kumbe sio uwezo wao mdogo bali ni fikra potofu tu waliojijaza katika ubongo wao ni wakufeli, uwezo wao mdogo hawawezi kufaulu kama wengine.

Daima kwenye masomo yako jijengee wewe ni mtu wa mafanikio na sio mtu wa kushindwa amini na unakili na uwezo  wa juu wa kufanya kuyafikia malengo katika masomo yako, amini Mungu amekupendelea kamwe asingekuumba kiumbe dhaifu.

Kuna msemo unasema “If you think you can,you can ;and if you think you cant, you cant.You are always right”.

Kuwa na imani ya kupata mafanikio kwenye masomo yako na si vingenevyo, usiwaze kushindwa kumbuka chochote unachopanda katika subconconsous mind kinafanyiwa kazi,”The subconscious mind makes no dstiniction between constructive and destructive thought impulses.

It works with the material we feed it,through our thought impulses.The subconscious mind will translate into reality a thought driven by fear just as readily as it will translate into reality a thought driven by courage or faith”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post