Jezi sita za Messi kuuzwa bilioni 25

Jezi sita za Messi kuuzwa bilioni 25

‘Jezi’ sita alizozivaa mchezaji kutoka ‘Klabu’ ya Inter Miami, Lionel Messi katika kombe la dunia akiwa na ‘timu’ yake ya Taifa ya Argentina ziko kwenye mnada wa takribani dola milioni 10 ambazo ni sawa na tsh 25 bilioni.

Katika ‘jezi’ hizo sita zitakuwepo ‘jezi’ mbalimbali alizotumia katika michuano hiyo ikiwemo alizovaa kipindi cha kwanza katika fainali, nusu fainali, robo na za mechi ya 16 bora dhidi ya Australia na nyingine mbili za michezo ya hatua ya makundi.Kupitia ukurasa wa Instagram wa Messi ameeleza kuwa sehemu ya mapato kutokana na mnada huo utapelekwa katika hospitali ya watoto ya Sant Joan de Déu (SJD) iliyoko Barcelona ili kukidhi mahitaji ya watoto wanaougua magonjwa adimu.

Mnada huo unatarajiwa kufanywa katika mtandao wa Sotheby's kuanzia Novemba 30 - Desemba 14.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post