Jeraha la shingo sababu ya Usher kuhairisha show

Jeraha la shingo sababu ya Usher kuhairisha show

Baada ya mashabiki kukerwa na Usher kuhusiana na tamko lake la kuhairisha show kwa lengo la kupumzika, hatimaye msanii huyo amefunguka sababu kuu iliyomfanya ahairishe show hizo kwa kudai kuwa amepata jeraha shingoni wakati akifanya mazoezi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana Alhamisi Agosti 15 amedai kuwa alipata jeraha shingoni wakati wa mazoezi hivyo inambidi kuhairisha matamasha yote kuanzia ya Ijumaa na Jumamosi na mengineyo ili aweze kupata muda wa kupumzika na kupatiwa matibabu.

“Matumaini yangu yalikuwa kwamba kwa tiba ya mwili na matibabu, ningekuwa na uwezo wa kushinda jeraha hilo na kuwa tayari kwa usiku wa ufunguzi. Kwa bahati mbaya, jeraha bado halijapona, na madaktari wangu wameamuru nisiimbe kwenye maonyesho yoyote wiki hii.”

Hata hivyo mshindi huyo wa Grammy mara nane aliongezea kwa kudai kuwa madaktari wake wamemwambia atakuwa sawa mpaka Agosti 20 mwaka huu.

“Habari njema ni kwamba madaktari wanasema kuwa kwa kupumzika na matibabu sahihi, nitakuwa tayari kuanza ziara yangu huko Washington DC tarehe 20 Agosti. Nawapenda mashabiki wangu na ninawashukuru kwa kuelewa kwamba jeraha hili lazima lipone ili niweze kuwapa burudani kwa asilimia 100” ameandika Usher






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags