Jenerali Koome apiga marufuku maandamano, Kenya

Jenerali Koome apiga marufuku maandamano, Kenya

Mkuu wa polisi nchini Kenya Inspekta jenerali Japhet Koome amepiga marufuku wafuasi wa upinzani kuitisha maandamano haramu leo Jumatano kufuatia wimbi la hasira juu ya ongezeko la kodi iliyotangazwa na serikali ya Rais William Ruto.

Baada ya kiongozi wa upinzai Raila Odinga kuwasihi Wakenya kuingia mitaani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha, na watu watatu waliuawa kufuatia maandamano katika miji kadhaa siku ya Ijumaa.

Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini humo iliomba kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu matukio yote yaliyoripotiwa ya ukatili wa polisi, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International yakilaani watu kukamatwa kiholela.

Aidha Koome amesema walioandaa maandamano hayo hawakutoa taarifa zozote kwa polisi kuhusu maandamano yao yaliyopangwa wiki hii anasema.

“Kutokana na hilo, maandamano hayataruhusiwa hivi leo njia zote za kisheria zitatumika kusambaratisha maandamano hayo,” alisema inspekta huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags