Jela miaka 30 kwa kubaka, Njombe

Jela miaka 30 kwa kubaka, Njombe

Aloooooh! Haya matukio itafute namna ya kuyakomesha maana yamezidi kuongezea basi bwana, Mahakama ya Wilaya ya Njombe imemuhukumu Atanas Nzalalila (26) Mkazi wa Mahove Halmashauri ya Mji wa Njombe kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Msichana mwenye umri wa miaka 13 Mjini humo.

Katika shauri la jinai namba 60/2022, Mahakama imeeleza kuwa Mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 26/03/ 2022 katika Mtaa wa Mahove kinyume na kifungu cha sheria 130(2)(e) na 131(1) sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Njombe Isack Mlowe huku Wakili wa Serikali Andrew Mandwa akiwakilisha upande wa Jamhuri.

Duuuuuuh! Nini kifanyike kukomesha matukio haya ya kikatili huu dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags