JE WAJUA: Si kosa askari kukuta hauna leseni

JE WAJUA: Si kosa askari kukuta hauna leseni

Aiseee ulikua unaifahamu hii???

Kwa mujibu wa Sheria, sio kosa endapo askari akikuomba leseni kisha ukawa hauna kwa wakati huo.

Kupitia mahojiano, mdau wa jukwaa la Sheria ndani ya tovuti JamiiForums.com anatoa elimu kuwa askari wa usalama barabarani anapomuomba dereva leseni barabarani kama akiwa hana kwa muda huo sio kosa Kisheria. Anaeleza "Licha ya Kifungu cha 77 cha Sheria ya usalama barabarani kumtaka dereva wa chombo cha moto kutembea na leseni, lakini Kifungu cha 77(1) cha sheria hiyo kinasema dereva ana muda wa siku tatu za kutoa au kuonesha leseni yake, akishindwa hapo ndipo linaweza kuwa kosa." Mdau anasema "Sheria imetoa ahueni hii ikizingatia mazingira ya ubinadamu, huwezi kukumbuka leseni muda wote."

Licha ya hivyo, ni kweli Kifungu cha 77 cha Sheria ya Usalama Barabarani kinamtaka kila mwendesha chombo cha moto kutembea na leseni barabarani. Ni kweli askari anayo mamlaka kumsimamisha mwendesha chombo cha moto.

Na ni kweli pia kuwa askari ana mamlaka ya kumtaka mwendesha chombo cha moto aonyeshe leseni yake.  Lakini ambacho si kweli hata kidogo ni kuwa mwendesha chombo cha moto asipoonyesha leseni kwa wakati huo basi tayari ametenda kosa, si kweli.

Kifungu cha 77(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani kinasema kuwa mtu hatatiwa hatiani, kwa maana ya kulipa faini au kuandikiwa kosa au kuadhibiwa na chombo chochote ikiwamo mahakama, kwa sababu tu hakubeba, au hakutoa/kuonyesha leseni pale alipotakiwa kufanya hivyo, isipokuwa ana siku tatu za kutoa au kuonyesha leseni hiyo tangu siku hiyo aliposimamishwa.


Chanzo Jamii Forum, Jamhuri






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags