JE WAJUA kukosa usingizi wa kutosha kunapunguza nguvu za kiume

JE WAJUA kukosa usingizi wa kutosha kunapunguza nguvu za kiume

Ebwana eeh! haya si maneno yangu mimi bali ni utafiti uliofanywa na jarida linalochapisha habari za Afya LiveScience unasema kuwa  Wanaume ambao hulala chini ya saa sita wanaweza kutungisha Mimba kwa 31% huku wanaolala kwa saa tisa wakiwa na 49%.


Madaktari wanasema Mwanaume anachukuliwa kuwa amepata usingizi wa kutosha usiku iwapo atalala kwa kati ya Saa saba mpaka tisa. Hata hivyo, wengi hawazingatii hilo kutokana na shughuli za kutafuta riziki

Aidha Utafiti uliofanyika kwa Wanaume 2,676 wa zaidi ya umri wa Miaka 67 huko Marekani ulibaini kuwa  wale ambao hukosa usingizi wa kutosha hukumbwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume

Ebwana eeeh!! Ndugu zangu mnalala vizuri lakini au mnalalamika tu kuwa mnatatizo ilhali chanzo kinasababishwa na wewe wenyewe? Tuendee kumfuatilia hili.

Utafiti umeonesha kukosa usingizi wa kutosha kunapunguza uzalishaji wa Mbegu za Kiume na kukosekana kwa hamu ya mapenzi na ashki wakati wa Tendo la Ndoa

Aloooooh unaweza kudondosha comment yako hapo chini kuhusiana na utafiti huo vipi unaonaje hilo suala?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags