Daktari wa Magonjwa ya binadamu kutoka Hospitali ya Anglikana, iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam, Dk. Rahel Mwinuka anafunguka na kusema
Magonjwa ya Zinaa, ni magonjwa yaenezwayo kwa njia ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa, kutotumia Kinga wakati wa kujamiana na mtu aliyeathirika nayo.
Hata hivyo magonjwa haya ya zinaa huambukiza pia kupitia mama mjamzito kwenda kwa mtoto na njia nyingine nyingi.
Dalili nyingi za magonjwa ya kujamiiana, zinaendana na magonjwa mengine mengi kama maambukizi kwa njia ya mkojo (UTI), Fangasi za sehemu za siri nk.
Maambukizi ya magonjwa ya kujamiaana yana dalili nyingi, miongoni mwa dalili hizo ni kama ifuatavyo:-
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kutoka maji maji yasiyo ya kawaida sehemu sehemu za siri yenye rangi ya manjano, Kijani, yanayoweza kuwasha na kutoa harufu mbaya.
- Maumivu chini ya Kitovu
- Kujisikia kukojoa mara kwa mara
- Kuwashwa sehemu za siri
- Maumivu wakati wa kujamiiana
- Vidonda, upele na malengelenge kuzunguka uume, uke hata njia ya haja kubwa
- Uvimbe unaouma kwenye uume, Uke na hata Korodani
- Kutokwa damu wakati au baada ya kujamiana
- Hedhi sisizo na mpangilio
Kumbuka dalili hizi zitajirudia mara kwa mara, kama maambukizi yatakua ugonjwa na kukosa tiba sahihi.
Inashauriwa wenza kupima mara kwa mara hata kama dalili hazionekani kwa macho. Tunashauri watu wasipende kupima mkojo tu pindi waonapo dalili kama hizo, tunapaswa kupima zaidi ili kuzuia maambukizi kuingia kwenye ugonjwa.
Hata hivyo vijan wanashauriwa kuwa makini sana pindi wanapoamua kuanzisha mahusiano mapya ya kimapenzi.
Leave a Reply