Jaymoe: Msisubiri mpaka tufe ndio mtupe maua yetu

Jaymoe: Msisubiri mpaka tufe ndio mtupe maua yetu

Mkongwe wa Hip-hop nchini Jaymoe amewataka mashabiki na wapenzi wa muziki kumpa maua yake kabla hajafa kutokana na mengi aliyoyafanya na wasanii wenzie katika tasnia hiyo.

Katika ukurasa wake wa Instagram ame-share picha akiwa ana TID Mnyama ikiambatana na ujumbe ukiwataka mashabiki kuwapa maua yako kabla hawajafa.

“Jumah as @jaymoefamous na Khaleed as @tidmusic wote watoto wa mzee Mohamed, ndugu katika sanaa tangu tunakua mpaka sasa tunazeeka, tumefanya mengi ya kukumbukwa, kuanzia Zeze, Girlfriend Movie, Girlfriend Soundtrack, Mpenzi Kwaheri, Chumvini, Tingisha, inatosha kusema, sisi ni nguli hai. Usisubiri mpaka tufe ili kutupa maua yetu”

Kufuatia na kauli hiyo baadhi ya wasanii wamejitokeza katika upande wa ‘komenti’ na kuwamwagia maua yao akiwemo Joh Makini akiandika “Kinging for decades (Mfalme kwa miongo kadhaa)”, G Nako akiandika “Haipingwii wakuu wa bomaaa” na wengineo.

Utakumbuka kuwa Jaymoe ametamba na ngoma zake kama ‘Kimya Kimya’, ‘Pesa Ya Madafu’, ‘Nisaidie Kushare’ na nyinginezo huku ngoma yake ya mwisho ikiwa ni aliyoshirikishwa na Foby iitwayo ‘Tuliachanaje’ iliyotoka Julai 4 mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags