Jay Z ahofia watoto wake tuhuma za ubakaji

Jay Z ahofia watoto wake tuhuma za ubakaji

Mwanamuziki Jay-Z alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza akiwa na familia yake katika onyesho la Disney la Mufasa la ku premier filamu ya 'The Lion King' huko Los Angeles, Marekani tangu atuhumiwe kumbaka msichana wa miaka 13 mwaka 2000.

Katika filamu hiyo Blue Ivy (12) ambaye ni mtoto wa kwanza wa Jigga na Beyonce ni miongoni mwa waigizaji katika filamu ya The Lion King.

Hata hivyo, itakuwa mara ya kwanza kwake kuonekana katika filamu hiyo mpya huku akitambulika kwa jina la 'Kiara'. Kwa upande wa Beyoncé (43) katika filamu hiyo anarudia jukumu lake kama Nala, mama Kiara.

Jay Z ameendelea kuonesha namna alivyoguswa na tuhuma zinazomkabili huku hofu yake kubwa ikiwa kwa watoto wake hususani Ivy ambaye umri wake ni mkubwa na wa kuhoji vitu.

“Huzuni yangu pekee ni kwa familia yangu mimi na mke wangu, itabidi tukae chini na watoto wetu, mmoja wao akiwa katika umri ambao marafiki zake hakika wataona vyombo vya habari na kuuliza maswali juu ya chanzo cha madai haya, na kuelezea ukatili na uchoyo wa watu,"alisema Jay Z.

Hata hivyo Beyonce ameonesha kufurahishwa na mwanaye kwa hatua hiyo aliyofikia kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Mtoto wangu wa kike mrembo huu ni usiku wako. Ulifanya kazi kwa bidii na ulifanya kazi nzuri kama sauti ya Kiara. Familia yako inajivunia. Endelea kung'aa," aliandika Beyonce.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags