Jangwa labadilishwa kuwa Msitu

Jangwa labadilishwa kuwa Msitu

Kama tunavyojua kila Binadamu huishi na kufanya ayapendayo, hivyo hivyo kwa Hikmet Kaya, aliyekuwa msimamizi wa Misitu ya Kituruki aliamua kubadilisha jangwa na kuwa msitu ambapo wazo hilo lilimjia mwaka 1978.

Zaidi ya miaka kadhaa Kaya amekuwa akishirikiana na ‘timu’ yake na wanakijiji wa eneo analoishi kwa kupanda miti zaidi ya milioni 30 kwa lengo la kubadilisha mandhari ya ukame yaliyokuwa yametawala katika Wilaya hiyo.



Mzee huyo ameibua hisia za wadau wengi kupitia mitandao ya kijamii baada ya ku-share picha iliyokuwa ikionesha awali kabla hawajapanda miti na sasa, ambapo watu wamempongeza kutokana na kujitoa kwa bidii na kupinga ukataji wa miti katika eneo hilo. Lakini pia umekuwa mfano wa kuigwa ulimwenguni kote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags