Jamie Foxx aiomba mahakama kutupilia mbali kesi inayomkabili

Jamie Foxx aiomba mahakama kutupilia mbali kesi inayomkabili

Mwigizaji kutoka Marekani Jamie Foxx ameiomba mahakama kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa dhidi yake na mwanamke aliyemshutumu kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Kwa mujibu wa tovuti In Touch imeeleza kuwa nyaraka zilizofikishwa mahakamani na wakili wa mwigizaji huyo zinaeleza kuwa endapo Foxx alifanya kitendo hicho basi ilikuwa ni makubaliano ya wote wawili.

“Kama Jamie alihusika na kitendo chochote kama kinavyodaiwa katika kesi ya Doe, basi mwanamke huyo alikubali vitendo hivyo, vile vile na kama Jamie alifanya kitendo chochote kama ilivyodaiwa basi vitendo hivyo havikuleta hatari wala madhara yaliyopelekea kujeruhiwa”

Zaidi ya hayo, katika hati hiyo iliyofikishwa mahakamani Jamie alibainisha kuwa mwanamke huyo aliwahi kufungua kesi inayofanana na hiyo mwaka 2020, lakini ilitupiliwa mbali kutokana na vitendo vya uongo.

Hata hivyo Jamie aliiomba mahakama kufuta kesi hiyo huku akitaka gharama zake zote za kisheria zirejeshwe.

Ikumbukwe kuwa Novemba mwaka jana Jane Doe alimshitaki muigizaji Foxx kwa kudai kuwa alitumia silaha kumtishia kisha kumshika sehemu za siri mwaka 2015 katika mgahawa wa kifahari wa NYC.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags