Jake Paul awajia juu wanaokosoa pambano lake

Jake Paul awajia juu wanaokosoa pambano lake

Jake Paul amewajibu watu wanaosema kuwa Mike Tyson ni "mzee sana" kwa pambano lake, Akizungumza na Babcock kwenye kipindi cha TMZ Sports TV mapema wiki hii, alisema kuwa bondia huyo nguli ni mtu mzima na anaweza kufanya maamuzi yake mwenyewe.

Mahojiano hayo yanakuja baada ya Tyson, ambaye anatarajia kufikisha umri wa miaka 58 mwishoni mwa mwezi huu, kuahirisha pambano hilo hadi Novemba kutokana na masuala ya kiafya.

Wawili hao awali walipangwa kupigana Julai hadi Tyson alipopatwa na kidonda cha dharura wakati wa safari ya ndege kutoka Miami kwenda Los Angeles Mei 26.

"Ingawa ilibidi tuahirishe pambano hilo, nitaendelea na mazoezi muda si mrefu. Nashukuru wafanyakazi na matabibu ambao walinishughulikia, pia nashukuru kwa waandaji wote kwa kufanya kazi kwa bidii kutafuta tarehe bora na kupanga upya pambano hilo." Tyson alisema katika taarifa iliyonaswa na ESPN. "Wakati tuna tarehe mpya, matokeo yatakuwa sawa bila kujali wakati tunapigana, Jake Paul anapigwa nje nje."

 

( Imeandikwa na @masimba_tz )
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags