Jaji atupilia mbali kesi ya Drake

Jaji atupilia mbali kesi ya Drake

Baada ya kuhusishwa katika kesi ya vifo vya watu 10 vilivyotokea katika tamasha la Astroworld lililofanyika mwaka 2021, hatimaye Jaji Kristen Hawkins ametupilia mbali kesi hiyo dhidi ya Drake.

Katika tamasha hilo Drake alikuwa mgeni maalumu ambapo alialikwa na ‘rapa’ Travis Scott’ ambaye ndiyo mwenye tamasha hilo, ambalo lilizua taharuki baada ya umati wa watu kuongezeka wakati wanamuziki hao wakitumbuiza na kuwafanya watu wakose pumzi na kupelekea kufariki huku wengine kujeruhiwa.

Kutokana na madhara hayo familia za watu 10 waliofariki pamoja na majeruhi waliamua kuwashitaki Scott, Drake pamoja na promota wa tamasha hilo Live Nation.

Drake amefutiwa mashitaka hayo kutokana na kutohusika katika uandaaji wa tamasha hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags