Iphone 14 kuanza kuuzwa Tanzania leo

Iphone 14 kuanza kuuzwa Tanzania leo

Oooooh! Haya haya kumekucha kumekuchwa wale vipenzi vya apple phone kuna ujumbe wenu hapa, basi bwana unaambiwa Simu mpya za iPhone 14 zimeanza kuuzwa rasmi nchini Tanzania leo November 3 kupitia Msambazaji aliyepewa idhini ya kuuza bidhaa za APPLE aitwae iStore istoredar duka namba 15 Mlimani City, jijini Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa iPhone 14 hizo ambazo zinapatikana katika matoleo yake yote, zilichelewa kuingizwa sokoni Tanzania na Msambazaji huyu kutokana na zoezi la kuzihakiki na kutazama utendaji kazi wake kwa kutumia mitandao ya simu ya Tanzania.

Matoleo ya iPhone 14 yaliyoanza kuuzwa Dar es salaam leo ni iPhone 14, iPhone 14 Plus, iPhone 14 Pro, iPhone 14 Pro Max japokuwa zipo pia iPhone 13, iPhone 13 Pro, Pro Max, iPhone SE na iPhone 12.

"iStore ndio Wawakilishi wa Apple hapa Tanzania hivyo Mteja anaponunua bidhaa hiyo anapata uhakika wa asilimia 100 kuwa ni genuine na anapewa na waranti ya miaka miwili”

Haya wale wanao tamba kuwa wako na iphone 14 mko wapi, maana bongo ndo kwanza zinafika leo, umetapeliwa ukiwa wapi embu dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags