Inonga azua gumzo baada ya kutetema kama Mayele

Inonga azua gumzo baada ya kutetema kama Mayele

Hahahahaha! Make hapa kwanza ncheke, kama inavyo julikana wawili hawa Mayele na Inonga wakiwa katika ardhi ya Tanzania wanakuwa mahasimu, kufuatiwa na klabu zao wanazo zichezea kuwa na ushindani mkubwa.

Kumekuwa na minong’ono mingi kupitia mitandao ya kijamii baada ya Henock Inonga kwenda kushangilia mtindo ule anaoutumia Fiston Mayele wa kutetema.

Tukio hilo limetokea jana baada ya Mayele kuiweka bao la pili katika timu yake ya Taifa la DR Congo kwenye kufuzu Afcon 2023 ambapo walikuwa wanacheza na Goban, na kufanya Taifa zima kutetema kama ilivyo kawaida yake.

Balaa linakuja kupitia gumzo mitandaoni dhidi ya mwamba Inonga kutetema kama Mayele, je kwa upande wako unaona alifanya sawa au alizingia mwamba huyo kutoka klabu ya Simba dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags