Infantino: hakutakuwa na kadi ya blue

Infantino: hakutakuwa na kadi ya blue

Rais wa shirikisho la ‘soka’ Duniani (FIFA) Gianni Infantino ameweka wazi kuwa hakutakuwa na ‘kadi’ ya bluu katika mpira wa miguu.

Infantino ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa #IFAB nchini Scotland ambapo alieleza kuwa Fifa inapingana kuwepo kadi za bluu, kutokana na hapo awali hawakuwa na uelewa wa ‘kadi’ hiyo.

Ikumbukwe kuwa ‘Bodi’ ya Shirikisho la ‘soka’ Kimataifa (IFAB) lilipendekeza kuwepo kwa ‘kadi’ hiyo ambayo inampa mwamuzi nafasi ya kumtoa mchezaji uwanjani kwa dakika 10 kisha kumrejesha tena mchezoni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags