Ikulu yatoa tamko, Biden kuanguka jukwaani

Ikulu yatoa tamko, Biden kuanguka jukwaani

Ikulu ya Marekani ‘White House’ imesema kuwa Rais Joe Biden yuko sawa baada ya kujikwaa na kuanguka jukwaani alipokuwa kwenye sherehe za kuhitimu Chuo cha Jeshi la Wanaanga huko Colorado Marekani.

Biden alielekeza kitu ambacho kilikuwa kimeshika mguu wake kilichomsababisha aanguke ambacho kinafanana na mfuko mdogo wa mchanga.

Baada ya kuinuka alionekana kuwa vizuri, akitembea bila msaada huku akitabasamu.

Biden (80) alianza kukimbia, akitoka mahali alipokuwa akitoa hotuba kwa wahitimu wa chuo hicho. Tukio ambalo lilitumia zaidi ya dakika 90 kutoa stashahada na kuwapongeza mamia ya wanafunzi.

Alipokuwa akielekea kwenye kiti chake, alijikwaa na kuanguka chini. Rais alitua kwenye nyonga yake ya kulia kabla ya kuinuka ambapo maafisa wake, ikiwa ni pamoja na afisa wa Chuo cha Jeshi la Anga, walishika mikono ya Biden kumsaidia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags