Hellow wanangu wa Mwananchi Scoop. I hope mko good kabisa. Leo bwana katika biashara, nimekujia na jambo muhimu ambalo unatakiwa kulifahamu wewe mjasiriamali na mfanyabiashara ili mambo yasiende kombo.
Wengi wapo kwenye biashara hata hivyo hujiita wajasiriamali. Hii ni kwa sababu kumekua na mchanganyiko mkubwa kuhusu nani haswa ni mjasiriamali na nani mfanyabiashara. Sasa leo ndo utaamua na kuchagua uende upande upi
Tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiliamali ni hizi!
- Tofauti katika malengo makuu
Mjasiriaali ingawa anaweza kunufaika yeye kama yeye kutoka na anachofanya, lengo lake la msingi huwa sio yeye kama yeye afanikiwe bali lengo lake ni kuona suluhu fulani ya tatizo ambalo anataka kulitatua. Hivyo basi mjasiriamali hujikita zaidi katika jamii kuangalia nini anaweza kufanya cha kuleta ahueni.
Mjasiriamali huhamasika zaidi na vile ambavyo anaweza kutatua changamoto fulani. Kwa upande wa mfanyabiashara lengo kuu ni kupata faida, hakuna mtazamo wa kina kuhusu changamoto gani au kwa namna gani jamii husika itapata ahueni. Ingawa anachofanya mfanyabiashara kinaweza kutibu changamoto fulani, lakini hilo sio wazo lake kuu na sio ambacho haswa kimemuingiza katika biashara. Yeye kinachompa hamasa kweli ni kupiga hela fasta fasta.
- Utofauti katika ubunifu wa kufanya kazi
Mjasiriamali hujihusisha zaidi na kubuni bidhaa au huduma mpya na namna mpya ya kuwasilisha bidhaa na huduma zilizopo na kuzifikisha kwa namna ya kipekee sokoni. Unaona katika kila jambo mjasiriamali hujihusisha na upya fulani (jambo jipya).
Kwa upande wa mfanyabiashara, yeye hujishughulisha na vitu ambavyo tayari vimekwisha buniwa bila kuongeza kitu cha ziada. Hii ni kwa sababu lengo la mfanyabiashara ni kufanya chochote kile kitakachomuingizia faida. Mfano kaona mwingine anauza nguo na zinatoka basi nae atakwenda kufanya biashara hiyo hiyo ya kuuza nguo.
- Utofauti katika kupata hasara
Kwakua mara nyingi mjasiriamali ni mwanzishaji wa bidhaa au huduma mpya ya kufikisha bidhaa au huduma iliyopo katika soko jipya au ambalo tayari lipo, mara nyingi mjasiriamali huwa katika hatari kubwa sana ya kupata hasara ukizingatia huo upya wa kufanya jambo, watu wanashindwa kumwamini na kuamini bidhaa zake kwa haraka.
Lakini kwa upande wake mfanyabiashara ingawaje nae anaweza kupata hasara katika shughuli yake, hatari yake ya kupata hasira haiwezi linganishwa na mjasiriamali kwakua yeye mfanyabiashara ana husika na bidhaa au huduma ambayo tayari imekwisha fahamika, utaratibu wake wa jinsi ya kutengeneza na kuuza so yeye anakuwa anaaminika zaidi.
- Utofauti katika uhusiano na watu wa karibu katika shughuli
Mjasiriamali kwakua ana lengo la kutengeneza kitu fulani na mtazamo wake upo katika jamii, mara nyingi hujikita katika kutafuta timu bora ya kufanya nayo kazi, kwakua mjasiriamali ana mtazamo mpana wa kuona kitu alichonacho kinafika mbali na anajua bila watu wazuri wa karibu yake hatoweza.
Wakati huo mfanyabiashara kwakua hujikita zaidi katika kutafuta faida na yeye mara nyingi manufaa yake binafsi ndio jambo la msingi zaidi, huwa hatilii maanani sana mambo ya mahusiano na kukua kwa pamoja na wale anaofanya nao shughuli yake.
Mjasiriamali huboresha na kuzingatia hata mahusiano yake na mteja na mfanyakazi ni sehemu muhimu ya biashara wakati kwa mfanyabiashara mteja ni mtu tuu wa pembeni, wa nje ya biashara yake na wafanyakazi kama tuu watoa huduma wa kumnufaisha yeye mfanyabiashara afikie malengo yake.
Alooooh! Natumai umejifunza mengi na kunufaika kwa hayo machache tulio kueleza, basi usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii inayopatikana kwa jina la @Mwananchiscoop.
Leave a Reply