Ijue adhabu ya kumpa kilevi mtu aliyekwisha lewa

Ijue adhabu ya kumpa kilevi mtu aliyekwisha lewa

Leo tutaelezana juu ya adhabu iliyopo kwa mujibu wa sheria ambayo mtu anaweza kupewa endapo atampatia mtu aliyekwisha lewa kilevi kingine.

Wakili kutoka taasisi ya Avis Legal, Hamza Jabir anasema kuwa kwa mujibu wa sheria ya vileo ya mwaka 1968, ni kosa kwa mmiliki wa bar, pub, club au muuza vilevi yoyote au mtumishi wake kumuuzia mtu kilevi ilihali mtu huyo tayari amekiwsha kulewa.

Wakili Jabir, anasema adhabu ya kosa hilo kwa mujibu wa sheria ni faini au mtu kwenda jela mwaka mmoja au kutumikia vyote kwa pamoja.

Mwajiriwa asipofanya kazi ipasavyo adhabu hii inakuhusu

Tunaendelea kujuzana sheria mbalimbali katika kona hii.

Hapa tutaelezana adhabu ambayo mwajiriwa atapewa pindi asipofanya kazi zake kwa namna ipasavyo.

Wakili Jabir anasema ni kosa kwa mwajiriwa yeyote kuzubaa na kutokufanya kazi zake kwa namna impasavyo kwa kujishughulisha na mambo yake binafsi.

Anasema adhabu ya kosa hilo ni faini au kifungo cha miezi mitatu jela au vyote kwa pamoja na hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai na kanuni za adhabu sura ya 16.

Ukimwibia mume au mke wako jela miaka saba

Pia Jabir anafafanua kuwa kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16, ni kosa kwa mume au mke kumuibia mwezi wake kitu chochote ambacho ni mali yake halali mfano pesa kwenye pochi au mifuko ya suruari na koti.

Wakili Jabir anasema adhabu ya kosa hilo kwa mujibu wa sheria ni kifungo cha miaka saba jela.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags