Ifahamu Hotel hatari zaidi duniani

Ifahamu Hotel hatari zaidi duniani

Tunajua umeshazoea kutembelea katika hotel zenye vivutio mbalimbali vya aina yake lakini sijui kama unafahamu kuhusiana na hotel hatari zaidi duniani ambayo ipo katikati ya bahari ya Atlantic.

Hotel hiyo iliyopewa jina la ‘Frying Pan hotel’ imeelezwa kuwa hatari zaidi kutokana na umbali wa maili 34 kutoka pwani ya Cape Fear, North Carolina, ambapo hapo awali eneo hilo lilikuwa ni kituo cha taa cha zamani cha Walinzi wa Pwani ya Marekani ambacho kilibadirishwa kuwa hotel mwishoni mwa mwaka 1970.

Ili kufanikiwa kufika katika hotel hiyo unatakiwa kutumia usafiri wa ‘Helkopta’ au mashua pekee, hata hivyo ndani ya hotel hiyo kuna vitu vya muhimu vikiwemo sehemu ya maji moto ya kuoga, umeme, wifi, jiko, sehemu ya kulala nk.

Kwa siku tatu ndani ya hotel hiyo inagharimu dola $1,550 ambayo ni zaidi ya tsh 3.9 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags