Huyu Ndio Crush Wa Aaron Pierre Mufasa
Mwigizaji anayewakosha kinadada wengi kwenye mitandao ya kijamii Aaron Pierre ‘Mufasa’ amesema mwanamuziki na mwigizaji Ashanti ndiye mwanamke aliyekuwa akimvutia zaidi ‘Crush’.
Kupitia mahojinao yake na podcast ya Seasoned ya BuzzFeed, Aaron amesema wakati akiwa mdogo ndiyo alikuwa akivutiwa na nyote huyo.
“Crush wangu wa kwanza wa utotoni alikuwa Ashanti, na wa pili alikuwa Foxy Brown,” alisema Aaron
Mbali na hilo alifunguka kuwa yeye ni mtu mwenye mapenzi ya kweli lakini kwa sasa ameamua kuulinda moyo wake na yupo hivyo kila siku.
“Najiambia ukweli, mimi ni mpenzi wa kweli. Lakini kwa upande mwingine, nafikiria, kama wengi wetu, mimi ni mlinzi wa moyo wangu na mambo ya moyo yatabaki ndani yangu,”amesema Aaron
Aaron amekuwa katika vichwa vya habari kufuatiana mwonekano wake pamoja na filamu inayoendelea kufanya vizuri ‘Mufasa: The Lion King’ ambayo akiingiza sauti ya Mufasa katika filamu hiyo.
Ashanti ni mwanamuziki mwenye umri wa miaka 44 amewahi kutamba na ngoma kama Rain on Me, Unfoolish, Baby, Pac’s Life huku akionekana kwenye filamu kama Coach Carter, John Tucker Must Die, Bride and Prejudice na nyinginezo.
Leave a Reply