Uchunguzi bado unaendelea Los Angeles katika kesi inayomkabili rapa ASAP Rocky, ambaye anakabiliwa na mashtaka mawili ya uhalifu, akidaiwa kumpiga risasi rafiki yake wa zamani na mshirika wa kundi la muziki la ASAP Mob.
Hapo jana Januari 21, 2025 Rocky alifikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo lakini alikana na kisha aliachiwa kwa dhamana kwa sharti la kutowasiliana na mshtaki wa kesi hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na Nancy Dilon ambaye ni ripota wa Rolling Stone anasema mwanasheria wa ASAP Rocky, Joe Tacopina alithibitisha kuwa yeye na mteja wake wanapanga kuwaita mashahidi wawili ambao watasema bunduki iliyoonekana kwenye video ilikuwa ambayo Rocky aliibeba kwa sababu za kiusalama.
Kutokana na sheria za mahakama na uzito wa kesi hiyo iwapo atapatikana na hatia rapa huyo wa New York 'ASAP Rocky' ambaye jina lake halisi ni Rakim Mayers, anaweza kufungwa jela miaka 24.
Leave a Reply