Historia ya mchekeshaji Kantoroke

Historia ya mchekeshaji Kantoroke

Mambo vipi watu wa nguvu? Shukrani za dhati zikufikie mtu wa nguvu kwa support yako na kuendelea kufatilia story zetu kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii na jarida letu la Mwananchi Scoop, shout out kwako mwanangu wa nguvu!

Katika kulisaka tonge kuna mengi hutokea ikiwa pamoja na kudharauliwa, kuchekwa pia kukata tamaa lakini waswahili walisema mchumia juani hula kivulini. Naam! week hii katika burudani bhana nakusogezea mwamba kutoka tasnia ya uchekeshaji, Kantoroke maarufu kama "Nimekumaindi".

Kama tunavyojua tasnia ya uchekeshaji inakua kwa kasi ingawa watu wanaichulia pouwa na kutoipa thamani na kuifanya kazi rasmi kama kazi zingine za sanaa hivyo kupelekea jamii kuwa na mtazamo wa tofauti kwa watu wanaojihusisha na sanaa hiyo katika utafutaji wa ugali. Msanii Kantoroke ameeleza nyakati alizopitia kupambania ugali wake kupitia uchekeshaji, changamoto na maisha yake nje ya uchekeshaji na stori yake inaweza kuwa chachu kwako mtu wa nguvu katika kuchochea jitihada zako katika utafutaji.

Ally Muhidin maarufu kama Kantoroke ni mzaliwa kutoka mkoa wa  Tanga ambaye alianza sanaa ya uchekeshaji mwaka 2017 huku akiwa anafanya shughuli za ujasiriamali hukohuko jijini Tanga.

"Mwaka 2017 nilianza kurekodi video za vichekesho kwenye simu kisha na post mtandaoni ingawa sikuipa uzito sana sanaa ya uchekeshaji, ukizingatia nilikuwa mkoani hakuna mtu anayeweza kunijua ndo maana nikajihusisha sana na ujasiriamali,"alisema Kantoroke.

Palipo na nia siku zote kuna njia, baada ya video za vichekesho kuonekana mtandaoni na comment za watu zikampa nguvu zaidi kusimamia sanaa ya uchekeshaji na hata kufanya uamuzi wa kuja Dar es salaam kwa lengo la kufanya komedi.

“Nikaamua kuja Dar es Salaam kwa lengo la kufanya komedi kutokana na wachekeshaji wengi na fursa zitokanazo na komedi ziko nyingi tofauti na mkoani’’alisema msanii huyo.

Vilevile mwamba huyo akaendelea kwa kusema, “Sikuwa na ndugu wala sehemu ya kufikia hivyo ikanibidi nikae guest house kwa siku 12 na katika wakati huo niliwatafuta wasanii kadhaa wa komedi ili niweze kuzungumza nao na kuweza kufanya nao kazi.”

Msanii huyo akamalizia kusema katika kipindi hicho aliuza vitu vyake vya gharama kama TV, radio na deki ili aweze kupata pesa ya  kujikimu kimaisha, vilevile amefunguka changamoto analizokutana nazo katika kuikuza talanta ya uchekeshaji ambapo alisema,

“Vitu vinavyokwamisha msanii kukua ni pamoja na meneja kutokuwa na msimamo na kutanguliza maslai yao kwanza ukizingatia tasnia yetu ya komedi bado haijapata soko kubwa sana.”

Vilevile alisisitiza watu kuipa uzito komedi kama ilivyo sanaa zingine pia kutofautisha uhalisia au maisha ya mtu akiwa katika mazingira ya kazi maana inakuwa changamoto katika suala la mahusiano.

Haya mwanangu wa nguvu, usikate tamaa kupigania unachokiamini ili kufikia malengo yako. Hakuna jambo la rahisi hasa katika kuusaka ugali kupitia Sanaa, inahitaji kujituma, upendo kwa wasanii wenzako na ubunifu pia unaweza pata mahaojiano yake yote kupitia channel ya mwananchi digital YouTube.

Until next time byee byee!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags