Historia ya kundi la Zabron Singers hadi umauti kumfika Marco

Historia ya kundi la Zabron Singers hadi umauti kumfika Marco

Moja ya kundi la muziki wa injili linalofanya vizuri nchini ni hili la Zabron Singers kupitia baadhi ya nyimbo zao kama vile Moyo, Uko Singel?, Naogopa, Mkono wa Bwana, na Sweetie Sweetie
Kundi hilo ambalo limeingia kwenye majozi ya kufiwa na mmoja wa waimbaji aitwaye Marco Joseph, Jumatano Agosti 21 kutokana na ugonjwa wa moyo, limekuwa likifananishwa na kundi kutoka Rwanda liitwalo ‘Ambassadors Of Christ Choir’ ambao walitamba na nyimbo kama ‘Kwetu Pazuri’.
Kundi hilo awali lilikuwa lina jumla ya waimbaji 17 kutoka familia moja, lakini kwa sasa wamebaki 16 baada ya Marco kufariki dunia. Lilianzishwa mwaka 2006 Makao Makuu yake ni Shinyanga wilayani Kahama likiwa chini ya kanisa la Kisabato Kahama Central SDA.
Kutokana na mzee wao mkubwa aitwaye ‘Zabron’ kupendelea kuimba kwaya hivyo watoto, wajukuu na ndugu wengine wakaamua kuenzi kipaji na jina lake kwa aina hiyo ya kutengeneza nyimbo za kuabidu na kumtukuza Mungu.

Katika kipindi cha miaka 18 ya kundi hilo wamefanikiwa kutoa albumu tatu ya kwanza ikiwa ni ‘Nawakumbuka’ iliyotoka mwaka 2012 ikiwa na jumla ya nyimbo 11 ya pili ikiwa ni ‘Mkono wa Bwana’ 2015 na ya tatu ikiwa ni ‘Sio Bure’ yenye nyimbo 9 ambayo imetoka mwaka 2018.
Wimbo wa ‘Mkono wa Bwana’ ulivyochukuliwa kwa ukubwa
Ukiambiwa utaje nyimbo tatu za kundi hilo huwezi kuacha kuutaja wimbo ambao uliowaleta mjini ‘Mkono wa Bwana’ ambapo kwa mujibu wa mtunzi wa nyimbo za kundi hilo Japhet Zabron kwenye moja ya mahojiano yake aliwahi kusema kupitia wimbo huo kweli wameuona mkono wa bwana kwani ulichukua takribani mwaka mmoja mpaka wimbo huo kutrendi

“Mengi ambayo bwana alikuwa anatundea nyuma hata sasa amekuwa akitutendea ni mkono wake hali iliyofanya tukaandika wimbo huo. ulikuwa ni wakati ambao tunaongea na bwana na kutaka aongee na watu wake wote bila kujali aina ya dini, kabila wala rangi ndipo tukauona Mkono wa Bwana.

“Hakika mkono wa Bwana tumeuona, namna ambavyo tumegusa hisia za mashabiki na kubadilisha mienendo yao inabadilika na kutenda matendo mema hivyo kwetu ni faraja na tunaamini wengi wanauona mkono” amesema Japhet Zabron

Hata hivyo aliongezea kuwa wimbo wa Mkono wa Bwana ulitungwa mwaka 2013, kurekodiwa mwaka 2014 na kuachiwa rasmi mwaka 2015 lakini ulikuja kupokelewa vizuri 2016.
Ukiachilia mbali kusikilizwa, kutazamwa na kutumbuiza kwenye show kadhaa moja ya mualiko ambao ulikuwa mkubwa katika kundi lao ni waliopata katika uapisho wa Rais wa Kenya William Ruto uliofanyika Septemba 13, 2022.

Mbali na hayo Marco ambaye kwa sasa ni marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho Kahama mkoani Shinyanga. Apumzike kwa amani






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags