Historia ya hilda Baci mpishi alievunja rekodi ya dunia

Historia ya hilda Baci mpishi alievunja rekodi ya dunia

Amkenii!!! Team Scoop inatambua uwepo wenu wanetu wa faida na ndio maana kila weekend lazima tuwe tuna jambo na nyie wakurungwa tena katika segemeti hii ya michezo na burudani.

Leo katika segment kunakitu cha tofauti kidogo, najua mlipata kumuona na kumsikia mpishi alievunja record ya dunia kwa kupika muda mrefu na mapishi mengi kutoka nchini Nigeria.

Nina imani wanetu mnataka kujua historia ya huyu mwanadada shupavu na uwezo alio uonyesha, msicho kijua huyu dada ni maarufu na mwenye mafanikio kupitia social media kwa kuyatangaza mapishi yake mimi nasemaje kula chuma hicho!!!

Hilda Effiong Bassey, anayejulikana kama Hilda Baci, alizaliwa mnamo Septemba 20, 1996, katika jimbo la Akwa Ibom, kusini mashariki mwa nchi ya Nigeria, licha ya umri wake mdogo, Hilda amekuwa mpishi na mjasiriamali aliyefanikiwa kwa bidii yake.

Maisha yake yote yapo katika mji wa Akwa Ibom kwani huko ndiko anakotoka lakini alimaliza elimu yake ya upili katika chuo kikuu cha Madonna Okija, ambapo alipata shahada ya kwanza katika Sosholojia.

Mwaka wa 2020, alianza safari yake katika tasnia ya upishi bila mafunzo rasmi, lakini talanta yake ya asili na ubunifu vilimfanya atengeneze vyakula vitamu ambavyo vilivutia watu wengi.

Hilda alizindua chapa yake ‘Myfoodbyhilda’ ambayo ilianza na eneo moja lakini imepanuka hadi matawi kadhaa kote Nigeria. Akiwa Mkurugenzi mtendaji na mkuu wa mpishi wa restaurants yake ya  Myfoodbyhilda,

Hilda amelenga kutoa ubora, uvumbuzi na ubora katika chakula chake, hapa nikizungumzia ubora niweke msisitizo kwasababu kuna wale wenzangu na mimi kwenye sekta ya mapishi wanadharau sana lakini usmarti na ubunifu wa mtu unaweza ukaboresha mapishi yako.

Pia anashiriki kipindi cha kupika kupitia chaneli yake ya YouTube, ambapo yeye hutengeneza na kushiriki video za matukio yake ya upishi.

Mbali na kuwa mpishi na mjasiriamali, Hilda pia ni mtayarishaji wa TV, mwigizaji na mtangazaji mwenye talanta, ametayarisha na kukaribisha vipindi kadhaa vinavyohusiana na vyakula ikiwemo "The Hilda Baci Show" na "Myfoodbyhilda TV".

Kupitia maonyesho hayo Hilda haonyeshi tu ustadi wake wa kupika bali pia anashiriki shauku yake ya chakula na maono yake kwa mustakabali wa tasnia ya chakula ya Nigeria.

Leo hii amekuwa kinara wa mapishi ulimwengu na hiyo inatufanya tuamini kwamba amependa kupika na kujifunza kuboresha ujuzi wake wa upishi lakini hakuna habari kuhusu alijifunza wapi kuboresha ujuzi wake wa upishi na kuwa mpishi ambaye leo anashikilia Rekodi ya Dunia ya Guinness.

Aprili 2023, Hilda aliweka rekodi mpya katika mbio (marathon) ya siku nne za kupika, akivunja rekodi ya hapo awali iliyowekwa na Chef Lata London huko Rewa nchini India mnamo 2019 ambayo ilidumu kwa masaa 87 na dakika 45.

Mafanikio ya Hilda yanaonyesha kujitolea kwake kwa ufundi wake na azimio lake la kufanikiwa katika tasnia ya upishi.

Kitu ambacho mnatakiwa mjue hilda ni miongoni mwa warembo ambao wanathamini muonekano wao japo nimpishi alishawahi kufanya upasuaji (surgery) katika mwili wake ilikujiweka umbo namba nane kama wafanyavyo mabinti wengine hiyo ilizidi mfanya awe na muonekano wa kuvutia hasa katika vipindi vyake.

Hii inadhihirisha kuwa usidharau kile ambacho unacho na unaweza ukakiona kidogo au hakuna mtu alie wahi kufanya la hasha mtu mwenywe ndio wewe anza sasa mwanetu na wengine wa toe mfano au kuiga kupitia kwako.

Hilda huyo kashaweka record ya dunia kwasababu ya kupika ana kula mpunga wake kwanguvu yake na jasho lake kupitia talanta yake ya upishi wewe unasubiri nini amka sasa upambanie ndoto zako.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags