Hilda avunja rekodi ya dunia kwa kupika masaa 100

Hilda avunja rekodi ya dunia kwa kupika masaa 100

Mwanadada hilda kutoka nchini Nigeria amevunja record ya dunia ya Guinness kwakupika masaa 100, mrembo huyo ameivunja record ya masaa 87 na dk 45 iliyokua inashikiliwa na mwanadada Lata Tondon kutoka nchini India.

Hilda alikua na dk 5 tu zakupumzika kwenye kila lisaa na alitakiwa kupika chakula nakugawa watu wale sio kuuza, mastar wakubwa na viongozi kutoka nchini humo wamejitokeza kwenye mgahawa wake nakumpa saport mpaka jioni hilda alipofikisha masaa 100 jikoni.

Mpishi huyo mwenye talanta ya juu mwenye umri wa miaka 27 aliifanya Nigeria kujivunia kwa kushinda shindano hilo na kuondoka na zawadi kuu ya $5000.

Ikumbukwe tu Tondon kwa upande wake alivunja rekodi na kupata mafanikio hayo baada ya kupika kwa saa 87, dakika 45 na sekunde 00 mnamo mwaka 2019.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags