Hifadhi kubwa ya madini adimu yagundulika Sweden

Hifadhi kubwa ya madini adimu yagundulika Sweden

Hifadhi kubwa zaidi barani Ulaya ya madini adimu ambayo hutumiwa kutengenezea simu janja na makombora imepatikana nchini Sweden.

Hakuna madini adimu yanayochimbwa Ulaya kwa sasa na waziri wa Sweden alisifu ugunduzi huo kama njia ya kupunguza utegemezi wa nchi za umoja wa Ulaya EU kwa China.

Takriban asilimia 98% ya madini adimu yaliyotumika katika nchi za EU mnamo 2021 yaliagizwa kutoka China.

Zaidi ya tani milioni moja zimeripotiwa kupatikana kaskazini mwa Sweden. Ikitajwa kuwa ni sehemu ya akiba ya tani milioni 120 za madini adimu duniani, kulingana na makadirio ya Marekani.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post