Haya hapa usiyoyajua kuhusu mkali wenu, safari yake ya mapenzi

Haya hapa usiyoyajua kuhusu mkali wenu, safari yake ya mapenzi

Msanii wa vichekesho nchini Jackson Supakila 'Mkali Wenu' amesema katika vitu ambavyo watu hawavijui kuhusu yeye ni kutopenda kuwa kwenye mahusiano na wanawake wengi.

Akizungumza na Mwananchi amesema kutokuwa na tabia hiyo kulimfanya asijaribu kuzini hadi pale alipoingia kwenye ndoa mwaka 2022.

"Katika vitu ambavyo watu hawajui kuhusu mimi siyo mtu wa wanawake kabisa mimi niliwahi kuoa mwaka 2022 ndiyo mwanamke wangu wa kwanza kufaya naye tendo la ndoa tukazinguana mwaka 2024.

"Tangu hapo sijawahi tena kubahatika kufanya tendo na mwanamke mwingine kwa sababu hata vitabu vya dini vinasema tusiikaribie zinaa ukiniona na wanawake ujue nafanya nae kazi mimi hata nikitongoa mwanamke siwezi kufanya nae hadi nimuoe,"amesema

Anasema kutokana na hayo amekuwa akiwashangaa baadhi ya vijana ambao wanapena ujauzito kabla ya ndoa. Huku kwa uoande wake anasema tayari amebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.

"Mimi namtoto mzuri sana, mitandao ya kijamii ina vitu vinadumu sijataka kumuweka huko mwanangu wa kiume nilimpata na mke wangu,"amesema

Licha ya hayo mwigizaji huyo siku za hivi karibuni alionekana kuingia kwenye upande wa mchezo wa ngumi ambako pia anasema ameingia kwa sababu ya kupenda mchezo huo na siyo vinginevyo

"Nimeingia kwenye 'professional boxers' sijaingia kwa ugomvi lakini nimeingia kwa sababu ya burudani tu na kujitafuta ni mchezo ambao naupenda japo mgumu,"amesema Mkali Wenu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags