Ebwanaaa eeeh!! Ni Ijumaa tulivu kabisaaaa ikiwa watu mbalimbali wakimalizia zoezi zima la sensa ya watu na makazi ambapo imeanza rasmi Agosti 23 2022, naam, turudi kwenye burudani sasa wikiendi hii bwana tumejipanga vizuri kabisaaa.
Bila shaka ukurasa wa burudani bwana tunakuletea taarifa za baadhi ya mastaa mbalimbali kupitia tasnia zote ikiwemo uigizaji, muziki, uandishi na utangazaji, bila kusahau ambao wametoka kwenye muziki na kuingia kwenye siasa.
Unaweza ukajiuliza mastaa hao je wanahabari gani? Sasa basi moja kwa moja tumekuandalia taarifa za mastaa ambao wamebahatika kuingia kwenye ndoa lakini pia ndoa zao hazina mikimiki yaani zimetulia kabisaaa bila skendo.
Je unawafahamu? Mwananchi scoop imeandaa taarifa hivyo kwa kuangalia baadhi ya mastaa ambao wametulia kwenye ndoa zao bila kuwa na maskendo au kiki kama ilivyo kwa wengine.
Moja kwa moja bwana tunapiga hodi mlangoni kwa Mwanadada ambaye ni mjasiriamali na mtangazaji, Zamaradi Mketema, ambaye amefunga ndoa mwaka 2018 ambapo hadi kufikia mwaka huu atakua amefikisha miaka 5 kwenye ndoa yake.
Zamaradi ambaye amefunga ndoa na Shabani Hamisi ambapo hadi sasa hakuna kiki wala skendo yoyote kwa wawili hao.
Nikukumbushe tu mnamo siku kuu ya Valentine day inayoadhimisha tarehe 14 mwezi 2 kila mwaka ambayo ni siku ya wapendanao, tunakumbuka mwanadada huyo alimfanyia surprise kubwa sana mume wake ndani ya jiji la dar es salaam kwa kumuweka kwenye bango mwenza wake maeneo ya Morocco, akionesha namna gani anavyompenda.
Bango ambalo liliambata na ujumbe wa huba kutoka kwa Zamaradi uliandikwa hivi.
“Acha dunia ijue nakupenda kiasi gani you are my King. Happy Valentine day my Love ,from your loving Wife,” ujumbe huo bwana uliwashangaza watu kwelikweli hususani kwenye mitandao ya kijamii tunaweza tuakasema hiyo siku ni Zama day, sio poa.
Tukiachana na ndoa hiyo bwana nakuletea hii hapa sasa msanii mchekeshaji wa kitambo sana, Lucas Mhuvile maarufu Joti ambaye alifanikiwa kufunga ndoa mwaka agosti 28, 2017 ambapo hadi kufikia mwaka 2022 atakuwa anatimiza miaka 6.
Joti alifunga pingu za maisha na mke wake kipenzi Tumaini Hassan katika kanisa katoliki Magomeni jijini Dar es salaam.
Tuanweza kusema pongezi kwa wanandoa hao kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndoa yao hatujapata kusikia wala kuona vitimbi vyovyote.
Namleta kwako bwana Mbunge wa Jimbo la Muheza Tanga, Hamisi Mwijuma maarufu Mwana FA, kiongozi makini ambaye nae ametulia kabisaa kwenye suala lake la ndoa.
Kama unakumbuka Mwana FA alianzia kwenye nyanja ya muziki na baaadaye kuingia kwenye masuala ya siasa.
Hamis Mwijuma alifanikiwa kufunga ndoa yake Juni 5 2016 na mkewe Helga ambapo ndoa hiyo ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki zake wa karibu akiwemo AY, Ommy Dimpoz, Dully Sykes na wengine wengi.
Bado tunaendelea kukujuza kuhusiana na mastaa ambao ndoa zao hazina mba mba mba wala maskendo na maisha yanaenda kama kawaida tofauti na wengine bwana.
Hapa namleta kwako mzee wa Jua kali wanamuita Uncle Zumo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kupitia sanaa ya uigizaji bila shaka tunadhubutu kusema kwake pia hakuna machokoro mageni.
Mohamed Kingara maarufu Uncle Zumo alifunga ndoa na Habiba Zumo wakiwa na zaidi ya miaka 8 hadi sasa, bila shaka hata wewe msomaji utakua unaliona hilo jinsi wawili hao walivyotulia ndoani.
Uncle Zumo na Habiba Zumo ambao pia ni wazazi wa binti mdogo ambaye ameingia kwenye tasnia ya ucheshi Mai Zumo ambaye pia anafanya vizuri kwenye tasnia hiyo.
Yap tunamaliza na Mama la mama, Mama Dangote mwenye bila shaka tunafahamu kuwa mama licha ya mambo mengi yaliyopita huko nyuma lakini mama huyo ambaye amefunga ndoa mwishoni mwa mwaka 2017 ikiwa na zaidi ya miaka 6.
Bi Sanura Kassim maarufu kama Mama wa Dangote alifunga ndoa na Uncle Shamte, licha ya kuwa na maneno na vijembe vingi huko mitandaoni ikisemekana kuwa mama dangote amemzidi Uncle Shamte kiumri lakini wawili hao wameweka pamba masikioni mwao na yakwao yanakwenda.
Ebwanaaa eeeeh!!! Bila shaka utakua umepata mwanga na mwangaza na tumekufichulia baadhi ya tu mastaa ambao wametulia kwenye ndoa zao na hazina mba mba mba.
Usikose kufuatilia makala za burudani kupitia jarida la Mwananchi Scoop na wiki ijayo itakua babkubwa zaidi. Usikoseee!!!
Leave a Reply