Hatma ya Ramaphosa kujulikana leo

Hatma ya Ramaphosa kujulikana leo

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema hatma yake itatokana na uamuzi wa Halmashari Kuu ya Chama tawala (NEC) kutokana na tuhuma anazokabiliana nazo.

Ramaphosa ambae pia atahudhuria mkutano huo uliopangwa kufanya leo hii, anakabiliana na tuhuma baada ya jopo la wataalam kubaini uwepo na uwezekano wa kukiuka kiapo chake kazini kwa kuhusishwa na upatikanaji wa mamilioni ya dola katika shamba lake binafsi.

Aidha mwenyewe mara zote amekuwa akikana kuhusika na uovu wowote na hadi wakati huu hakuna mashtaka yaliofunguliwa dhidi yake. Kikiso kazi cha chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC kilikutana jana Jumapili mjini Johannesburg kujadili ripoti inayomweka matatani Rais Ramaphosa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags