Hatimaye Vybz Kartel aachiwa huru, washabiki wajitokeza gerezani kumpokea

Hatimaye Vybz Kartel aachiwa huru, washabiki wajitokeza gerezani kumpokea

Leo unaweza kuiita sikukuu kwa wapenzi wa muziki wa ‘Dancehall’ ambao kwa asili unatokea Nchi ya Jamaica, ambapo mkali wa muziki huo Adidja Azim Palmer maarufu kama Vybz Kartel ameachiwa huru baada ya kusota kwa miaka 13 gerezani.

Staa huyo alikaa miaka mitatu akiwa mahabusu mpaka pale hukumu yake ya kifungo cha maisha ilipopitishwa Machi 13, 2014.
Kartel alihukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya Clive ‘Lizard’ Williams akishirikiana na wenzake watatu ambao ni ‘Shawn Campbell’, Andre St John na Kahira Jones.

Kartel ameachiwa huru baada ya miaka 13 ya mapambano kupinga kifungo hicho, ambacho kimepitia mabadiliko kadhaa baada ya kupatikana na hatia kwa kesi nyingine ya mauaji huko nyuma lakini kumekuwa na mkanganyiko mkubwa juu ya maamuzi ya rufaa yake hii na namna kesi ilivyoendeshwa kwa muda mrefu.

Vybz, ametajwa kujihusisha na makundi ya kihalifu na hivyo mfumo wa maisha yake kuwa ya shaka sana ingawa sasa yupo huru.
Mwanamuziki huyo katika kipindi cha miaka 13 aliyokaa jela, ameripotiwa kuachia ngoma nyingi kuliko wasanii wengi walio uraiani kwani alikuwa na ruhusa ya kufanya muziki licha ya kuwa kifungoni.

Sababu kuu ya kuachiwa huru wakati kifungo chake kikiwa kinaendelea inatajwa ni kutokana na hali mbaya ya kiafya inayotishia uhai wake ambapo alibainika kusumbuliwa na maradhi ya ‘Graves’ Disease’ yanayosababisha matatizo kwenye koo, moyo na saikolojia yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags