Kumekuwa na tabia baadhi ya watu wanakwepa kutoa taarifa zao sahihi pindi waendapo kupumzika kwenye nyumba za kulala wageni (Guest House), tena wapo ambao kudanganya taarifa zao wamefanya kama'fasheni', bila ya kujali kuwa kutotoa taarifa zao sahihi ni hatari kwa usalama wao.
Katika maeneo mbalimbali ya kupumzikia wageni, watu hukutana na maswali yanayohitaji taarifa zao binafsi wa ajili ya kujaza kwenye kitabu cha wageni kabla ya kukabidhiwa chumba, kati ya maswali hayo mtu huulizwa majina yake sahihi, umri, eneo atokalo, namba za simu, na wengine huenda mbali zaidi na kuuliza, kabila, kazi afanyayo mtu pamoja na mali alizobeba kwenye mabegi yake.
Kukwepa kutoa taarifa zako sahihi na kutoa za uongo kunaweza kukusababisha uingie katika matatizo ambayo yalikuwa hayakuhusu, mfano katika eneo hilo likatokea tukio la uhalifu na askari wakafanya msako kwenye vyumba, pindi jina la kwenye kitambulisho chako na kwenye daftari likiwa tofauti unaweza kujikuta unatiliwa mashaka kwa kudanganya taarifa zako.
Kushindwa kupata msaada wa haraka ukipata tatizo, kama ifahamikavyo matatizo hayagongo hodi na hakuna ajuaye kesho yake endapo utapata tatizo kama vile kifo, ugonjwa au kupoteza fahamu itakuwa ngumu kuwapata ndugu au marafiki wakukupa msaada kwani jina ulilotumia si sahihi ambalo watu wako wa karibu wanalifahamu.
Aidha kudanganya taarifa kutakupa ugumu wa kupata mali zako kwa haraka zilizopotea ukiwa kwenye nyumba hiyo, wakati mwingine ili uweze kupata ulichopoteza ni muhimu kuonesha uthibitisho wa uhalali wa umiliki wa mali iliyopotea, kutokana na kudanganya kwako kutasababisha ugumu kupata haki yako kwani taarifa za umiliki zitakinzana na za kwenye kitabu.
Hivyo basi hakikisha uendapo kwenye nyumba za kulala wageni unaandika taarifa zako kwa usahihi ili kuepukana na baadhi ya mambo yanayoweza kujitokeza eneo hilo.
Funguka huwa unaandaka jina sahihi ukienda kulala nyumba ya wageni?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply