Harusi yaingia doa, Moto waua watu 100 ukumbini

Harusi yaingia doa, Moto waua watu 100 ukumbini

Inadaiwa takribani watu 100 wamefariki na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa baada ya moto mkubwa kutokea ukumbini wakati wa sherehe ya harusi katika Wilaya ya Al-Hamdaniya nchini Iraq.

Mpaka kufukia sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu chanzo cha moto huo lakini ripoti za awali za kituo kimoja cha habari nchini humo kimeeleza kuwa huenda moto huo umesababishwa na fataki zilizokuwa zikirushwa kwenye ukumbi huo.

Bibi harusi na bwana harusi wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waathiriwa wa tukio hilo, ambapo sehemu ya jengo ilidondoka na kuwakandamiza watu wakati sherehe ikiendelea.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags