Harusi ya mtoto wa bilionea yakutanisha mastaa

Harusi ya mtoto wa bilionea yakutanisha mastaa

Kama wasemavyo waswahili binadamu ana sherehe tatu. Kwanza kuzaliwa, pili ndoa na tatu kufariki.

Kutokana na maana hiyo kwa upande wa mtoto wa bilione Mukesh Ambani, Anant Ambani na Radhika Merchant wameitendea haki sherehe yao ya pili.

Hii ni baada ya kufunga harusi ya kifahari huku ikihusisha watu maarufu duniani kama vile Shah Rukh Khan, Salman Khan, Deepika Padukone, na Amitabh Bachchan,Kim Kardashian, Mike Tyson, Adele, John Cena,Justin Bieber, Mark Zuckerberg, Khloe Kardashianna wengineo.

Kabla ya harusi hiyo ambayo imefanyika leo, Julai 12, kulikuwa na matukio ya yalijumuisha sherehe kubwa mjini Jamnagar, ambapo Rihanna alifanya onesho la kusisimua.

Pia, familia ilifanya sherehe nyingine ya kifahari nchini Italia Justin Bieber pia alihudhuria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags