Harmonize na Poshy wamwagana

Harmonize na Poshy wamwagana

Baada ya kutikisa kwenye mahusiano kwa takribani miezi saba, mwanamuziki Harmonize anadaiwa kutemana na mpenzi wake Poshy Queen, hii ni baada ya wawili hao kublokiana kwenye mtandao wa Instagram.

Ukiachilia mbali kukublokina na kila mmoja kumu-unfollow mwenzie pia kila mmoja amefuta picha pamoja na video ambazo wamewahi kupiga pamoja.

Wawili hao walianza mahusiano yao Januari 2024 ambapo kwa mara ya kwanza walionekana wakiwa pamoja wakati walipokwenda kutalii kwenye moja ya vivutio nchini.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa wawili hao kuachana kwa staili hii, kwani mwezi Februari kila mmoja alifuta picha na kumu-unfolow mwenzie lakini baada ya siku kadhaa Harmo na Poshy walirudiana tena.

Endapo watakuwa wameachana mazima basi haya yatakuwa mahusiano ya tano ya Konde kuvunjika ambayo amewahi kuyaweka mtandaoni akianzia na Jacqueline Wolper, Sarah Michelotti kutoka Ital, Kajala na Yolo The Queen kutoka Rwanda.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags