Harmonize na manjonjo uwanjani, kusitisha ushiriki game la Jumamosi

Harmonize Na Manjonjo Uwanjani, Kusitisha Ushiriki Game La Jumamosi

Msanii Harmonize 'Konde Boy' kumbe sio mziki πŸŽ™ pekee hata kwenye mpira ⚽ yupo vizuri na leo alikuwa kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa kwa ajili ya mechi ya Samakiba (Samatta + Ali kiba) itakayopigwa Jumamosi Juni 18.

Harmonize ameonesha mbwembwe zake uwanjani, hata hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliomba radhi kwa kutoweza kushiriki tena mashindano hayo.

Harmonize aliandika, "Changamoto & Mitihani & Shida Matatizo Mbalimbali Yapo Mengi Sana Katika Jamii Zetu Hata Uwe Tajiri Kiasi Gani Huwezi Maliza Shida Za Watu Wote ila Tusivunjike Moyo Katika Kutengeneza Faraja Kwa Wahitaji Hatakama Kwa Uchache Kiasi Gani Binafsi Nimefurahishwa Sana Na Hii Movement Ya Brothers Tanzania Football icon @samagoal77Pamoja Na Tanzania music icon @officialalikiba Binafsi Nilitamani Kushiri Sanaa Kwapamoja Ili Kutengeneza Furaha Zaidi Ila Naamini KONDEGANG F.C Mtaniwakirisha Hiyo Tarehe 18/6/ JUMA MOSSI Na Niwaambie tu Rasmi Kuwa Sisi Ni TEAM #SAMMATA Wana bahati Sanaa Ndo Hivyo Tuu Majukumu Ya kazi ..!!! Nayo Muda Mwingine Ukishakula Hela Za Watu ..!!! Ma Boss washakata Maticket Yao Huko Mjini GOMA CONGO Ila Ninaimani Msimu Ujao InshallahπŸ™ Tutakuwa Wote ..!!! CONGRATS TEAM MAANDALIZI Wanangu Twendeni Tuka Enjoy Twendeni Tukachangie Faraja Ya Wenzetu Waishio Mazingira Magumu ❀ #NIFUATE"

Anyway, bado tuna mategemeo makubwa sana kwenye game hii. Hongera kwao Samatta na Ali Kiba kwa kufanikisha hili.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post