Harmonize kunogesha tamasha la pili la Utamaduni la Kitaifa

Harmonize kunogesha tamasha la pili la Utamaduni la Kitaifa

Staa wa Bongo Flava, Hamornize leo Agosti 27 atatoa burudani kwenye kilele cha tamasha la pili la Utamaduni la Kitaifa linalofanyika katika Stendi ya zamani iliyopo Njombe Mjini.

Tamasha hilo lililoanza Agosti 25 limekuwa na shughuli na maonesho mbalimbali ya kitamaduni na sanaa likihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk Pindi Chana ambaye alitoa wito kwa mikoa na halmashauri zote nchini kuainisha na kutambua maeneo yote ya utamaduni katika maeneo yao, kuyaratibu na kuyahifadhi pamoja na kuyatangaza.

Kauli mbiu ya tamasha hilo ni utamaduni ni msingi wa maadili, tuulinde na kuuendeleza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags