Harmonize aachia orodha ya nyimbo za albamu yake

Harmonize aachia orodha ya nyimbo za albamu yake

Licha ya maneno kuwa mengi katika mitandao ya kijamii kuhusiana na shoo anazofanya nchini Marekani, msanii huyu wa kizazi kipya nchini ajulikanaye kwa jina la Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize ameachia 'Cover' pamoja na list ya nyimbo 20 ambazo zinapatikana kwenye albamu yake mpya ya ‘High School’.
Mkali hiyo ya hit song mbalimbali hapa nchini amefunguka na kusema kuwa albamu hiyo inatarajiwa kutoka Novemba 5 mwaka huu huku ikiwa na kolabo 6 pekee.
Kwenye albamu hiyo ya pili ya Tembo amewapa mashavu Sarkodie kutoka Ghana, Naira Marley (Nigeria), Busiswa Gqulu (Afrika Kusini) huku kutoka Bongo Ibraah, Anjella wote kutoka Konde Gang na Sholo Mwamba.
Unaambiwa mashabiki huko wamekaa mkao wa kula kuingojea albamu hiyo ambayo wanaamini itakuwa na vionjo mbalimbali vya muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags