Hali ya bishara za nguo msimu huu wa sikukuu

Hali ya bishara za nguo msimu huu wa sikukuu

Kama tunavyojua ni mwisho wa mwaka na kuna sikukuu kadhaa hapo mbele, ambapo watu wengi hujumuika pamoja kula, kunywa na kuvaa nguo mpya, kama ilivyo ada MwananchiScoop tumeamua kukusogezea washonaji na wauza maduka kutoka Kariakoo wao watatueleza kuhusiana na biashara kuelekea msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Waswahili wanasema kazi ni kazi kikubwa mkono uende kinywani, licha ya kuwa kuna baadhi ya watu wanadharau baadhi ya kazi za wengine bila kujali kuwa hiyo ndiyo kazi inayo muendeshea maisha.

Karne hii watu wengi wamekuwa wakidharau kazi ya washonaji wa cherehani lakini leo tupo hapa kupinga kauli hiyo kwa sababu tumekusogezea mshonaji mkubwa ambaye kwa upande wake kushona cherehani ilikuwa  kitu anachopenda tangu akiwa mdogo waswahili wanasema iko kwenye damu.

Kwa kuanza na muuzaji wa duka la nguo mchanganyiko kutoka Kariakoo jijini Dar es saalam aitwaye Salum Mohammed maarufu kama ‘Saloom Shop’ kwa upande wake ameweka wazi kuhusiana na muenendo wa biashara za nguo ulivyo kuelekea msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

“Kuelekea sikukuu hizi  kwa mwaka huu biashara siyo nzuri sana wala mbaya sana ilimradi tu tunapata pesa ya kujikimu na familia” amesema Salum

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa nguo zinazouzika kipindi hiki ni nguo za watoto huku akiweka wazi kuwa mpaka sasa bei za nguo ni zile zile bado hazijapanda.

Kama tunavyojua miaka ya nyuma kipindi kama hichi kwenye maduka Kariakoo kulikuwa hapatoshi kutokana na watu kufurika kwa ajili ya kununua nguo.

“Biashara miaka ya nyuma ilikuwa nzuri sana muda kama huu tulikuwa hatupumziki watu wanakuja na kutoka dukani lakini sasa hivi biashara imepoa sana siyo kama kipindi cha nyuma” amesema Salum

Wahenga walisema ukiona moshi unafuka kwenye kibanda basi ujue ndani moto unawake Bwana Salum ameeleza kuwa sababu ya watu kutonunua nguo katika sikukuu hizi za mwisho wa mwaka ni kutokana ugumu wa maisha na vitu kuzidi kupanda bei kila uchwao.

Hatukuishia hapo safari moja kwa moja mpaka kwa mshonaji wa nguo Mariam Said anayepatikana Kigamboni jijini Dar es salaam kwa upande wake amewataka watu wanaodharau kazi hiyo ya cherehani waache mara moja kwa sababu ni kazi ambayo inalipa kuliko watu wanavyofikiri licha ya kuwa kazi hiyo ni ya msimu.

“Tunashukuru Mungu biashara ni nzuri si msimu huu tuu kwa sasa watu wengi naona kama wamerudi katika dhama za zamani kuanza tena kushona vitambaa, kwa upande wangu mimi naona biashara hii imenilipa sana kuelekea sikukuu hizi” amesema Mariam

Si hayo tu ameweka wazi kuwa biashara kwa mwaka huu imekuwa nzuri kuliko hata miaka iliyopita watu wengi walikuwa wakikimbilia Kariakoo kutungua nguo dukani lakini mwaka huu umekuwa tofauti kwa upande wao na hii ni kutokana na watu kuvutiwa na baadhi ya mishono wanayoiyona kupitia mitandao ya kijamii.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags