Hajia4Real ashatakiwa kwa mapenzi ya ulaghai

Hajia4Real ashatakiwa kwa mapenzi ya ulaghai

Staa wa muziki kutoka  nchini Ghana Faiz Montrage, maarufu kama Hajia4Real, amerudishwa Marekani na kushtakiwa kwa kashfa ya mapenzi ya ulaghai wa dola milioni mbili.

Hajia4Real ambaye ni maarufu kupitia mtandao wa Instagram, alipokea pesa kutoka kwa watu kadhaa ambao walidanganywa kutuma pesa kama sehemu ya ulaghai wa mapenzi.

Sambasamba na kampuni ya uhalifu aliyo kuwa anaifanyia kazi mwanamuziki huyo inayodaiwa kufanya nayo kazi ikilenga hasa watu wazima ambao waliishi peke yao.

Aidha kampuni hiyo ilikuwa ikiwatumia barua pepe, ujumbe mfupi wa maandishi, na ujumbe wa mitandao ya kijamii, na kutengeneza utambulisho bandia ili kuanzisha uhusiano wa kimapenzi wa kitapeli.

Baada ya kutengeneza uaminifu kwa watu kushawishika kwa kisingizio cha uwongo, kuhamisha pesa kwa akaunti za benki zinazodhibitiwa na washiriki wa kampuni ya uhalifu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags