Haddish aliwahi kumtaka Leonardo kimapenzi

Haddish aliwahi kumtaka Leonardo kimapenzi

Mwigizaji wa Marekani Tiffany Haddish amewaacha hoi mashabiki baada ya kuweka wazi kuwa aliwahi kumuomba mkali wa Titanic Leonardo DiCaprio kuwa naye kimapenzi.

Tiffany ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano yake na podcast ya ‘The Howard Stern Show’ baada ya kuulizwa kuhusiana na mahusiano yake yaliyopita ndipo akadai kuwa aliwahi kumtamka Leonardo DiCaprio kimapenzi lakini mwigizaji huyo alikataa ombi hilo.

Aidha kwa mujibu wa Tiffany alidai kuwa aliamua kumtamkia ukweli Leonardo ili aweze kuwa naye karibu kwenye shughuli zao za uigizaji huku akiwaza kuwa huenda angepewa uhusika mkuu kwenye filamu ya zamani ya ‘What's Eating Gilbert Grape’.

Licha ya Leonardo kukataa ofa hiyo lakini Haddish anakiri kwamba bado ataendelea kumshawishi mwigizaji huyo ili aweze kuwa naye kwenye mahusiano.

Haddish hapo awali alikuwa kwenye uhusiano na rapper Common, uhusiano huo ulianza mwaka 2019 na kuachana mwaka 2021, lakini mpaka sasa bado hajaweka wazi uhusiano wake mpya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags