Habibu Suluo: Marufuku Mahubiri na Biashara kwenye Mabasi

Habibu Suluo: Marufuku Mahubiri na Biashara kwenye Mabasi

Kama kuna jambo linawakera baadhi ya watu basi ni hili la kufanya shughuri mbali mbali ndani ya usafiri yaani mabasi, hivyo basi Serikali limekemea kitendo hicho kupitia mamlaka ya Usafiri Ardhini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafi Ardhini (LATRA), Habibu Suluo amesema kwa mujibu wa kanuni ni marufuku kwa Wafanyabiashara na wanaohubiri dini kupanda kwenye mabasi na kufanya shuguli zao za biashara na mahubiri ndani ya mabasi .

Suluo ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanahabari leo July 26, 2022 Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.

"Ukipanda mabasi, utakuta Watu wanaingia kwenye mabasi kufanya biashara, utakuta wanaingia wanahubiri mambo ya dini kwakweli kanuni zetu zinakataza, tunakataza kwasababu sio mahali pake kwahiyo tunasisitiza biashara kwenye mabasi marufuku, wale wenye kutoa mahubiri kwenye mabasi ni marufuku, tuzingatie kanuni" amesema Habibu Suluo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags