Google Map yashitakiwa kwa kusababisha kifo

Google Map yashitakiwa kwa kusababisha kifo

Kampuni ya Google, upande Google map imeshitakiwa na familia ya Philip Paxson baada ya Google Map kusababisha kifo cha ndugu yao huyo aliyekuwa akisafiri kwa kutumia muongozo wa ramani ya Google, iliyompoteza na kumuelekeza sehemu isiyo sahihi yenye daraja bovu na kumsababishia ajali hadi kifo chake.

Kwa mujibu wa Sky news inaeleza kuwa Philip alikuwa akirudi nyumbani kwa ajili ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya binti yake akiwa anatimiza miaka 9, ambapo Septemba mwaka jana alifariki baada ya gari kutumbukia katika daraja huko North Carolina, nchini Marekani.

Familia ilieleza kuwa eneo alilokuwa akipita lilikuwa geni kwake ndipo alitumia ramani za Google iliyo muelekeza kuvuka kwenye daraja ambalo lilikuwa bovu na kusababisha gari yake kutumbukia.

Aidha familia hiyo inaishtumu Google kwa uzembe, na kudai kuwa kwa takribani miaka mitano kampuni hiyo ilikuwa ikipewa taarifa na watu kuwa daraja hilo limeanguka na waliitaka irekebishe taarifa za ‘ruti’ lakini kampuni hiyo haikufanya hivyo.

Inaelezwa kuwa ‘Polisi’ wa eneo hilo waukuta mwili wa Philip kwenye gari yake iliyokuwa imepinduka na kuzama chini ya daraja hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags