Gladnes Kifaluka Aweka Wazi Alivyo Pata Uchizi

Gladnes Kifaluka Aweka Wazi Alivyo Pata Uchizi

Mchekeshaji kutokea nchini Tanzania Gladnes Kifaluka ameweka wazi namna alivopitia wakati mgumu kwa kuugua uchizi na afya ya akiri kipindi cha ujauzito wake, ambapo kitaalamu inafahamika kama Postpartum.

Gladnes amesema hayo kwenye video aliyweka kupitia ukurasa wake wa instagram akiongelea hali hiyo aliokuwa akipitia wakati anaujazito ambapo alikuja kufahamishwa anatatizo hilo baada ya kuonana na daktari.

"Nilikuwa najisikia kujiuwa, nilikuwa nalia sana bila kujua tatizo ninini nakosa hamu ya kula lakini nilipo onana na Daktari alinambia bila kunificha kuwa nimeugua uchizi Mental health" amesema Gladnes.

Postpartum depression ni aina ya mfadhaiko au huzuni inayowapata baadhi ya wanawake baada ya kujifungua. Inahusishwa na mabadiliko ya homoni, uchovu, changamoto za uzazi, au hofu ya majukumu mapya. Dalili zake zinaweza kujumuisha huzuni ya kudumu, kukosa nguvu, kulia kupita kiasi, matatizo ya usingizi, hasira, au hata hisia za hatia na kutojiamini kama mama.

Ni hali inayohitaji msaada wa kiafya, kihisia, na kijamii ili mama apate nafuu na kurejea hali yake ya kawaida.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags