Future Adai Hajui Chochote Bifu La Kendrick Na Drake

Future Adai Hajui Chochote Bifu La Kendrick Na Drake

Rapa kutoka Marekani Future amedai kuwa hafahamu chochote kuhusu bifu la Kendrick Lamar na Drake.

Future ameyaeleza hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na GQ ambapo amefunguka kuwa alikuwa hajui kama kulikuwa na bifu na wala hakuwahi kushiriki kwenye bato zao.

“Kumbe kulikuwa na bifu? sikuwahi kufahamu kama kulikuwa na bifu. yaani sikujua chochote kinachoendelea na wala sikuwa kushiriki kwenye bato yoyote ya ku-rap jamani” amesema Future

Future ambae alishirikiana na Kendrick Lamar na Metro Boomin kwenye ngoma ya "Like That" ambayo ndio mzizi na chanzo cha bifu la Drake na Lamar ilitoka rasmi miezi saba iliyopita ikiwa na zaidi ya watazamani milioni 100 kwenye mtandao wa Youtube mpaka kufikia sasa.

Kupitia wimbo huo Kendrick aliwachana Drake na J cole akieleza kuwa hakuna wakubwa wa rap watatu marekani ila yupo mmoja ambaye ni yeye akiwa anapinga kauli J Cole aliyesema ma-rapa wakubwa Marekani kwa sasa ni watatu "Big Three" ambao ni J cole, Drake na Kendrick Lamar

"Like That" ikiwa kama ngoma ambayo ilitambulisha bifu la Kendrick na Drake imefanikiwa kuingia kwenye tuzo kubwa za Grammy 2025 kwenye kipengele cha "Best Rap Perfomance" tuzo ambazo zinatarajiwa kutolewa February 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags