Frida Amani Kukiwasha Sauti Za Busara 2025

Frida Amani Kukiwasha Sauti Za Busara 2025

Mwanamuziki wa Hip Hop na mtangazaji nchini Frida Amani anatarajiwa kufanya show katika tamasha la Sauti za Busara 2025, linalotarajia kufanyika kuanzia Februari 14 hadi 16.

Staa huyo ametangazwa kuwa mwana hip hop pekee kutoka Bongo ambaye atakiwasha siku ya Ijumaa Februari 14 huku akiungana na msanii mkongwe wa muziki wa Rumba, Christian Bella na Malaika Band.

Hayo yamewekwa wazi mapema leo Januari 21,2025 katika mkutano wa waandishi wa habari uliyofanyika jijini Dar es Salaam katika utambulisho wa tamasha la Sauti za Busara toleo la 22.

Wasanii hao ambao ni baadhi watakaowakilisha Bongo katika tamasha hilo wataungana na wasanii wengine kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Ukhoikhoi (South Africa), Boukuru (Rwanda), Assa Matusse (Mozambiqure), Blinky Bill (Kenya), Charles Obina (Uganda), Nidhal Yahyaoui (Tunisia) na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags