Mwanamuziki Frida Amani 'Madam President' wakati akifanya mahojiano na Mwananchi, leo Februari 15, 2025 amesema kinachofanya aandike historia kila mara kwenye muziki ni tabia yake ya kutojiwekea mipaka.
Frida ambaye jana Februari 14, 2025 aliingia kwenye historia ya kuwa msanii wa kwanza wa kike wa muziki wa Hip-hop kutumbuiza kwenye jukwaa la Sauti za Busara. Ni zao la mashindano ya kusaka vipaji BSS
" Mimi ni mmoja wa watu ambao nagonga hodi sana. Sijajiwekea vizuizi mimi nandoto kubwa, kuna vitu naviona kichwani natamani vifikie. Nawekeza sana muda wangu katika kufanya kazi,"amesema Frida.
Aidha msanii huyo anayetamba na nyimbo kama Madam President, Anakudanganya , Mi Nawe na Do you Wanna. Ambazo zote zipo kwenye mfumo wa masimuluzi, amesema aina ya utunzi wake unaendana na maisha yake alisi.
"Unajua muziki ulianzishwa, ulikuwa unaelezea stori za watu mimi siku zote kwenye muziki naamini watu wanatakiwa wapate stori fulani. Nimekuwa nikielezea zangu na za watu wengine na mashabiki wanapokea kwa ukubwa.
"Mfano wimbo wangu ‘Mi Nawe’ ni stori yangu ya ukweli nilikutana na mtu dukani nikampenda kweli, lakini kwa sasa tumeachana,"amesema Frida
Hata hivyo amesema ni muhimu kufanya uwekezaji kwa wasanii wa kike wanaopenda muziki wa Hip-hop ili waongezeke kwenye soko.
"Uwekezaji, ndiyo unakwamisha watoto wa kike. Mimi naamini inatakiwa waongezeke watu ambao wanaamini katika uwezo wa mtoto wa kike kwenye rap waweke hela. Wakiona mimi nikifika sehemu fulani itamsaidia hata yeye kuamini kuwa inawezekana,"amesema Frida
Hii siyo mara ya kwanza kwa Frida kuweka rekodi Mei 2024, alikuwa msanii wa kwanza kushiriki katika mkutano wa kimataifa ‘NEXT’ uliokuwa umeandaliwa na Kituo cha Utangazaji cha Uturuki ‘Turkey Radio Televisheni’ (TRT)

Leave a Reply