Foxx: Nilienda kuzimu na kurejea

Foxx: Nilienda kuzimu na kurejea

Muigizaji kutoka nchini Marekani Jamie Foxx amezungumza kwa mara ya kwanza tangu afya yake ilivyo anza kudhorota mwezi Aprili na kupelekea mkali huyo kukimbizwa Hospitali.

Kupitia video aliyo-post kwenye mtandao wa Instagram ameweka wazi magumu aliyopitia wakati akipambania afya yake.

Kupitia video yake Foxx amesema,
“Hata siwezi kuanza kukueleza umbali niliokwenda na jinsi nilivyorejea, nilihisi kama sikuwahi kamwe kufika hapo, Sikupenda unione hivyo. Nilipenda unione nikicheka, nikipata wakati mzuri, niki-party, nikifanya mzaha, nikiigiza filamu, kwenye kipindi cha televisheni. Sikupenda unione nikiwekewa mrija na kujaribu kujua kama nitavuka au lah!.”

“Lakini nilikwenda kuzimu na kurejea. Safari yangu ya kupona ilikuwa na vikwazo pia, lakini nimerejea na naweza kufanya kazi. Bila kusahau nawapongeza binti yangu Corinne na dada yangu Deondra Dixon kwa kutunza siri kipindi cha matibabu yangu mpaka kupona”
Kati ya movie alizocheza Foxx ni Day Shift akitumia jina la Bud Jablonski, Sleepless akiwa na jina la Vicent na nyingine nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags