Flaviana alaani matukio ya watoto kupotea

Flaviana alaani matukio ya watoto kupotea

Mwanamitindo Flaviana Matata ambaye pia aliwahi kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Miss Universe 2007 ambapo alifika Kumi Bora. Ameonesha kusikitishwa na matukio ya kupotea kwa watoto na kisha kupatikana wakiwa wametolewa baadhi ya viungo.

Flaviana ameeleza kuwa matukio hayo yanasikitisha na kuumiza

"Inasikitisha sana na kuumiza kuona matukio ya watoto kupotea na kupatikana wakiwa wameuawa na kukatwa baadhi ya viungo yanapamba moto. Watanzania tumekua watu wa aina gani jamani?," ameandika Flaviana

Utakumbuka kuwa hivi karibuni kuna tukio lilitokea Mbagala wilayani Temeke, Dar es Salaam, ambako Yusra Mussa, mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mbagala Kuu, aliuawa ikidaiwa baadhi ya viungo vya mwili wake, ikiwamo figo iliondolewa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilisema tangu Machi Jeshi hilo limepokea taarifa nne kutoka kwa wazazi wa Mbagala na Temeke na kati ya matukio hayo matatu yalisababisha vifo vya watoto waliotendewa ukatili.

Lakini Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alikana watoto hao kuondolewa viungo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags